Mama marehemu: Uavyaji mimba unavyowafanya wasichana wengi kuwa mama wasiokuwa na watoto

Jacinta* ana umri wa miaka  24 lakini hadi  kufikia sasa ameavya mimba mara sita .

Ni ufichuzi ambao hata yeye unamshangaza kwa sababu wakati wanapofanya kitendo hicho ,haja huwa kuondoa mimba haraka anavyoweza   kwa sababu anasema hayuko tayari kumlea mtoto wala hajaolewa na hivyo basi hana uwezo wa kuanza kuwa mzazi . je,ilinzaje mpaka ikawa mtindo kwake kuanza kuavya mimba?

Yote yalianza aakiwa shule ya msingi darasa la  nane akijitayarisha kufanya mtihani wa KCPE .kwa sababu ya shinikizo nyumbani kwamba ingekuwa aibu kwake kupata mimba akiwa shuleni na ukali wa babake ,mamake ndiye aliyempa ushauri wa kuitoa mimba hiyo na hapo ndipo alipomuua mtoto wake wa kwanza .Akifirikia kuhusu hilo na mimba zote alizotoa hadi sasa ,anasema  endapo angewazaa wote  basi angekuwa mama wa watoto sita! Ila hali sio hiyo kwa sababu yeye nini ama marehemu kama anavyosema mwenyewe .

Mimba za maepama sio jambo geni afrika a kuna tatizo kubwa sana la wasichana wa shule kuanza uzazi wakiwa na umri mdogo . matarajio ya wazazi na hofu za kifamilia zikizidishwa na kuharamishwa kwa uavyaji mimba ni jambo ambalo limesababisha kuongezeka sana kwa visa vya wasichana kuavya mimba .  Jacinta anasema wazazi wake hawakuweza kuzungumza naye kuhusu masuala ya upangaji uzazi au kufanya ngono na kinga na hivyo basi kila alipokuwa akishiriki ngono na wavulana wa rika lake ,alikuwa akijihatarisha kupata mimba ambayo hajapanga kuipata .

Anasema mimba zote alizotoa zilitokana na woga  wa jinsi wazazi wake na hasa babake angelichukulia suala la yeye kwa mja mzito .  Katika visa vyote alivyopata mimba ,wanaume waliokuwa wamempachika mzigo huo nao pia hawakuwa tayari kulea watoto hao na walikuwa wepesi sana wa kutoa pesa za kwenda kufanya taratibu za kuiavya mimba .Kutumia madaktari  wanaondesha oparesheni za kuavya mimba , hilo limekuwa jambo rahisi sana kwa sababu unapogundua tu una mimba kunao madaktari wanaokupa tembe za kuitoa na pia kufanya taratibu za kusafisha uzazi wako .

Jacinta anasema aliweza kujulishwa kwa daktari wa kliniki moja mtaani aliyekuwa akiwasaidia wasichana kutoa mimba na hapo ndipo uhusiano wao ulipoanza na kila alipompigia simu kwamba na uja uzito na alitaka kuutoa ,daktari huyo alikuwa tayari kumpa usaidizi aliohitaji .

Hata hivyo mwaka ajana Jacinta anasema alianza kupatwa na hofu ya maisha yake ya baadaye hasa atakapotaka kuolewa kwani alisikia kuna uwezekano kwamba mtu anayeavya imba huweza kupata tatizo la kuzaa tena baadaye.Hilo limempa msonono na baada ya kuanza kutumia  njia za upangaji uzazi ili kuzuia mimba amekuwa akiwaza sana kuhusu maisha yake ya ndoa na iwapo Mungu atamuadhbu wa mimba zote sita alizotoa