'Kama Mutula Kilonzo anataka kuning'atua amekaribishwa,'Kivutha Kibwana amwambia Mutula

Cheche za maneno zinazidi kushuhudiwa kati ya viongozi wa humu nchini huku kupitia kwenye mitandao ya kijamii,mnamo Jumatano gavana wa kaunti ya Makueni Kivutha Kibwana alimkaribisha Seneta wa kaunti hiyo Mutula Kilonzo amshtaki na kuwa kilisha mdahalo wa kung'atuliwa kwake kwenye kiti ch ugavana.

Huku bunge la seneti likishindwa kukubaliana kuhusu ugavi wa mapato, Kivutha alimuuliza Mutula kama anaweza ongoza kaunti bila pesa zozote kwa miezi mitatu.

Kupitia kwenye ukuras wake wa twitter Kivutha alikuwa na haya ya kusema,

"Kwa miezi mitatu seneti imekataza kaunti fedha za ugatuzi na mishahara, je gavana Mutula anaweza eneeleza kaunti bila fedha kwa miezi mitatu?

Kutimuliwa kwangu kama gavana kwa mwaka wa 2014 bado kuko kwenye seneti, seneta wa askari ambaye alinipiga risasi alifungwa

Iweje seneti kuangusha wananchi wa kenya kisha kuanza kulaumu magavana na rais?" Aliandika Kivutha Kibwana.

Huku akikashifu maseneta alisema kuwa baadhi ya wafanyakazi wa kaunti wameenda kwa ofisi yake kwa maana wamefungiwa nyumba kwa kutolipa kodi ilhali maseneta wanazidi kupokea mishahara yao.

https://twitter.com/governorkibwana/status/1306285771549282307

Pia Kivutha alimkaribisha Mutula awasilishe mdahalo wa kutimuliwa kwake kwa mara ya pili.

"Kama seneta Mutula Kilonzo anataka kunitimua kama gavana kwa mara ya pili amekaribishwa, nilisikia tishio ya kutimuliwa kwangu kutoka kwa chama cha Wiper kabla ya leo."

Akiwa kwenye mahojiano awali na radiojambo gavana huyo alidai kwamba atawania kiti cha urais mwaka wa 2022.