Bunge la seneti kuanzisha mjadala kuhusu mtandao wa kijamii wa Tik Tok

tiktok
tiktok
Bunge la seneti humu nchini litaanza mahalo mpya kuhusu utumiaji wa data wa mtandao wa kijamii wa Tik Tok, na wanamitandao wa humu nchini.

Hoja ilioletwa na seneta mteuliwa Iman Falhada Alhamisi wiki hii alisdai kuwa video zinazo pakiwa na mtandao huo zinaleta wasiwasi.

Mtandao huo kwa muda sasa umekuwa ukipokea ukosoaji jinsi data za wanamitandao katika mtandao huo zinatumika na hata ulinzi wake.

"Kamati ya kudumu ya habari na teknolojia kufanya kazi na mashirika ya serikali ili kuja na sera na mfumo wa kisheria kuhakikisha matumizi salama ya programu kama hizo na kulinda data za wakenya ambazo zinachukuliwa na programu hiyo ya Tik Tok

Kumekuwa na madai makubwa kuhusu dhidi ya programu hiyo kuhusu faragha ya data,Tik Tok imekuwa ikikusanya maeneo ya watumiaji mtandao huo,namba za simu,hata kuhusua habari nyingine za mitandao ya kijamii na umri wa mtumiaji." Alieleza Iman.