Diamond ampongeza Mbosso baada ya kupata kazi ya ubalozi

Msanii wa lebo wa WCB Mbosso amepata kazi ya ubalozi katika kampuni ya Tanga Fresh, huku akithibitisha habari hizo alishukuru kampuni hiyo kwenye ukurasa wake instagram.
Asante Sana kwa Kuniamini , Ahadi Yangu Kwenu Sitawaangusha na Hamtajutia Kufanya Kazi na Mimi ..

.. Si Mmetaka Wanywe Maziwa Ya Basi na Kuyaoga Watayaoga Mwaka Huu ... " 🤝. Mbosso Aliandika.

Mkurugenzi wa lebo ya WCB Diamond Platnumz alimponeza Mbosso huku akimwandikia ujumbe ufuatao;

Oooh Hoo Kumekucha!.......MBOSSO KHAN Official Tanga Fresh Brand Ambassador!!....Fanya Ufanyavyo kaka Balozi, ila chondechonde mi naomba usinisahau walau pakti tatu tu kwa wiki niwe nachanganyia Karanga zangu nikitaka Kuanza kutema Kwa Chumba..... 💣⛽🔥." Aliandika Diamond.

Baadhi ya wasanii wa lebo ya WCB walimpongeza na hizi hapa jumbe zao;

Romy Jons:SIJUI ITAKUAJE MWAKA HUUU!!!!. NIPITE SAA NGAPI VITU VANGU KAKA????

Official Tanga Fresh Brand Ambassador 🤝

Zuchu:KING KHAN more wins ,

Kim Kayndo :Hongera Sana Mufti. Hakika Huu Mwaka Ni Bora Sana Balozi Rasmi Wa Sema Cheti Sikupi Bila Carton Ya Maziwa 🤣🤣