NEMA yafunga kambi ya Mara Ngeche katika mbuga ya Maasai Mara

nyumbu
nyumbu
Mamlaka ya utunzi wa mazingira nchini (NEMA) imefunga kambi ya Mara Ngeche katika mbuga ya wanyama pori ya Maasai Mara.

Mamlaka hiyo imesema sababu za kufunga kambi hiyo ni kutokana hatia ya kukiuka kanuni za utunzi wa mazingira.

Katika ujumbe kwenye Twitter NEMA ilisema wamiliki wa kambi hiyo wameagizwa kubomoa majengo yote kutoka eneo hilo na kufanya upya utahmini kuhusu athari za kambi hiyo kwenye mazingira katika eneo hilo.

Mahema manne katika kambi hiyo pia yalipatikana kujengwa kinyume na kanuni za NEMA wakati maafisa wa mamlaka hiyo yalizuru eneo hilo.

Mjadala mkali iliibuka nchini baada ya video kuchipuka mitandaoni ikiwaonyesha wafanyikazi wa kambi hiyo wakiwafukuza nyumba waliotaka kwenda ng'ambo ya pili baada ya kuvuka mto Mara.

Waziri wa Utalii Najib Balala alikuwa ametoa agizo la kufungwa mara moja kwa kambi hiyo lakini siku kadhaa baadaye kambi hiyo ilikuwa bado inaendelea na shughuli zake kama kawaida.