Orodha ya wasanii waliopatikana na kashfa na kuwa kwenye vichwa vya habari

Tuliwasikia na hata kuwafahamu kupitia kwa vyombo vya habari baada ya kuhusihwa kwa migogoro tofautilicha ya kuwa wanamuziki wa nyimbo za injili na hata kuwa kwenye mstari wa kwanza kuwaonyesha mashabiki wao mfano mwema.

Baadhi ya wasanii waliojipata pabaya baada ya madai kuwa wamo na mgogoro au kupatikana kwa njia isiyostahili ni;

1.Ringtone Apoko

Apoko amekuwa kwenye vichwa vya habari mara kwa mara baada ya kupatikana upande usiostahili au kwa mambo yote mabaya.

Mwaka jana Ringtone alionekana kwenye mitandao ya kijamii akiwa amebeba bango la kumtafuta bibi ambapo si jambo njema hasa kwa msanii wa nyimbo za injili.

2.Bahati

Bahati amekuwa kwenye tasnia ya usanii kwa zaidi ya miaka mitano huku akifungua lebo yake iliyokuwa inafahamika kama EMB, kwa muda msanii huyo amekuwa kwenye mitandao ya kijamii wakizozana na wasanii wenzake

Huku kashfa ya kukamatwa kwake msanii Peter Blessings na aliyekuwa produca wake Paulo ikigonga vichwa vya habari kisha mengi kusemwa.

Msanii huyo pia ana Baby mama licha ya kumuoa Diana Marua, hivi sasa ndoa inaendelea vyema.

3. DK Kwenye beat

JIna lake lilifahamika na kufahamika sana wakati alidaiwa kumuambukiza msichana wa kutoka Nakuru na ugonjwa, msanii huyo alikubali makosa au madai hayo na kisha kuomba msamaha.

4.Weezdom

Alienea sana kwenye mitandao ya kijamii baada ya picha zake na mwanamke mmoja wakiwa kitandani kuibuka kwenye mitandao hiyo,mwanamke huyo alidaiwa kuwa wa msanii mwenzake.

Picha za wawili hao zilionekana walikuwa na mahabara ya mapenzi, kitandani.

5.Hope Kid

Kama vile msanii DK alishtakiwa kuambukiza msichana ugonjwa baada ya kufanya ngono naye, pia msanii Hope kid alikuwa kwenye kashfa hiyo  ya msichana huyo huku akiwekwa ndani.

Baadaye Hope kid alikubali makosa yake na kuomba msamaha.

6.Niccah the queen

Wazungu walisema methali hii'my dress my choice' msanii huyo mara kwa mara mavazi yake uwaacha wengi na maswali mengi huku madai ya kuwa kitandani na msanii Weezdom ikigonga vichwa vya habari.

7.Eko dydda

Uvumi ulienea sana kwenye enz zile kuwa msanii huyo amechana na mke wake, huku mkewe akidai mumewe si mwaminifu katika ndoa yao.

Kama msanii mmoja anapaswa kufanya nini ili kujitenga na kashfa tofauti hasa za ngono, ni kweli kila mmoja wetu ni binadamu na lazima tuwe na hisia lakini hisia nyingi zimefanya wasanii wengi kujipata pabaya.

Huku wengi wakilala korokoroni kwa ajili ya madai tofauti, kutokana na uchunguzi wangu wasanii wengi hutaka kutambulika sana huku ikiwabidi wengi kufanya mambo yasiyostahili na mambo hayo kufanya wajipate pabaya na muda kuwa ushaapita baada ya kufahamu walichokuwa wanataka kutenda au kufanya.

Je wanapaswa kufanya nini ili kujitenga na mambo kama hayo? Wengi wanapaswa kujipenda jinsi walivyo na kuridhika na chochote wanapata kama mapato ya na riziki yao ya kila siku.

Si wote ambao upenda kujipata mahali pabaya lakini bila kujua wanajipata upande huo huku wengi wakikejeliwa na kukosolewa vikali na wanamitandao na hata wakenya.

Si mmoja au wawili ambao waliwashangaza wengi baada ya habari zao kugonga vyombo vya habari bali baadhi ya wasanii wengi waliwashangaza mashabiki wao.