Seneta huyo aliiweka video yake mtandaoni akiwa akatika shamba la bangi katika taifa la Lithuania .
Olekina ambaye alikuwa nchini humo amesema iwapo Lithuania imehalalisha Bangi basi Kenya pia inafaa kurekebisha sharia ili kuhalalisha mmea huo ili kuwapunguza makali wagonjwa hasa wa ugonjwa wa saratani .
“ Mbona Kenya bado tumesalia katika msimamo wa zamani wa kuharamisha bangi …inanuka kama bangi..huenda nikalewa huu ndani’ Ole Kina amesema katika video hiyo .
Alizidi kusema “ iwapo mmea huu unaweza kupunguza uchungu kwa wagonjwa wa kansa basi tuuhalalishe ..ni kipi kibaya sana kuhusu mmea huu watu huishi mara moja tu’.
Mbunge wa zamani wa Kibra marehemu Ken Okoth alikuwa amepigania kuhalalishwa kwa bangi .Okoth aliwasilisha mswada wa kuthibiti bangi bungeni mwaka wa 2018 ili kuhalalisha mea huo .
Seneta wa Nairobi Mike Sonko aliasjhiria katika mazishi ya Okoth kwamba ingekuwa bora kuendleza kazi ya mbunge huyo kwa kuendelea kupigania kuhalalishwa kwa bangi ili iweze kutumiwa kwa matibabu