Mwanamke ajipata pabaya baada ya kukula 'fare' na kisha kushtakiwa na mwanamume huyo

Mwanamke mmoja alijipata pabaya baada ya kutumiwa nauli na mwanamume mmoja na kisha akaamua kuikula, ni visa ambavyo wanaume wengi yaani 'Boychild' amekuwa wakipitia endapo watamtumia mwanamke pesa ili asafiri kumtembelea lakini mwishowe anakula pesa hizo na kuzima simu.

Kwa mwanamke huyo alichezea mwanamume asiyechezewa na wengi baada ya kula nauli yake na kisha kuenda kumshtaki kwa kituo cha polisi.

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii mwanamke huyo alikuwa na haya ya kueleza;

"Nataka kufahamu kama kuna sheria ya kukula fare nahitaji ushauri wenu, huyu mwanamume ananitishia kwa maana nimekula fare ya elfu mbili alisema kuwa atatuma polisi waje kwangu hajali kama watakula pesa zake ili kukujia elfu mbili zao kwa maana anasema mimi ni tapeli." Alieleza Mwanamke huyo.

Huku akimalizia ujumbe wake alisema kuwa,

"Alinitumia OB kuwa kuna polisi watakuja kunibeba kama mbwa aliniambia kuwa amekabiliana na watu kama mimi, na tayari amelipa shillingi 2800 ili niwea kufuatwa

Je ushawahi kula kauli ya mwanamume na kisha mambo yakakugeukia?