Pyramid schemes
Palitokea makundi mengi mengi ya kuchanghisha na kuweka pesa kama akiba na hata mengine yakiahidi faida kwa kujisali nayo ili kuweka kiasi Fulani cha pesa baada ya muda Fulani . Pindi ilipojulikana kwamba watu wengi walikuwa kweli wamepokea faida , idadi hata Zaidi ya wakenya waliendelea kuziweka pesa zao katika mashirika hayo ambayo hakuna aliyejua mwanzoni kwamba yalikuwa ya walaghai .
Muda sio mrefu wamiliki wa mashirika hayo walifunga afisi zao na kukwepa na mamilioni ya pesa za wananchi . watu walipoteza akiba za miaka kadhaa kwani walitaraji kupata mafaao katika siu za baadaye .Kutoka mashirika kama vile DECI N na mengine ya akiba na mikopo ,wakenya wamekuwa waathiriwa wa kupunjwa fedha kupitia mipango kama hiyo ya kuzua shauku
Quail/Tombo na mayai yake
Asiyekumbuka sifa za mayao ya ndege huyu na nyama yake ni nani? Miaka michache iliyopita kuana waliozuka na madai kwamba ndeghe huyu na mayai yake ni miradi ambayo ingeleta mapato mengi sana na maelfu ya watu walikimbia hata kuchukua mikopo kuana kuwafuga ndege hao . mwanzoni ikaonekana kana kwamba kweli kulikuwa na pesa lakini baadaye wakati mayai ya tombo yalipojaa sokoni na bei ikatumbukia ,kila mkulima wa ndege hawa alikuwa akilia machozi ya majuto lakini hakuna aliyekuwepo kumliwaza . Inadaiwa waliokuja na madai hayo walikuwa washatengeza pesa za kutosha na kujiendea zao
Liquid screen protector
Huko mitaani na vijijini umewaona watu na vijisanduku vyemnye kemikali inayodaiwa kuweka kwenye simu ili kulinda kioo chako . Mwanzoni ,watu walikuwa wakitoa hata shilingi 2000 kuwekewa kemikali hiyo ya majimaji ili kuzikinga simu zao zisiweze kuvunjika vioo hata zikiangushwa . Kumbe wakati huo wote huu ni mchezo wa ulagjai na hadi leo kuna wakenya wasiojuwa kwamba ‘kinga’ hiyo ya simu haisaidii nab ado wanalipa pesa ili kuwekewa katika simu zao za mkononi .
Maski
Mwanzoni mwa janga la corona ,maski ama barakoa ilikuwa mojawapo ya bidhaa zilizokuwa na gharama ya juu . kuna aina moja ya maski za samawatu ambazo hutumiwa na madaktari ambazo ziliuzwa shilingi 300 mwanzoni mwa mwezi machi .Kufikia mwezi septemba maski hizo zilikuwa zikiuzwa shilingi tano! Maski zilipungua bei kw anjia ya kushangaza hadi imebainika kwamba kumbe kuna wafanyibiashara waliotumiua janga la corona kama chambo cha kujinufaisha kifedha .