‘Keki ya kitaifa inafaa kuongezwa’- Raila

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga amesema  magavana wanafaa kujipa jukumu la kuzidisha uzalishaji ili pawepo raslimali za kutosha kwa wakenya wote .

Raila  amesema keki ya kitaifa imekuwa ikipungua  huku akionya kwamba huenda pakatokea  janga endapo  hakuna kitakachofanywa ili kuhakikisha kwamba kila mkenya anapata raslimali a kujiendeleza hasa katika kaunti zote 47 .

“ Wananchi wetu na  viongozi wanafaa  kukugundua kwamba kuzidisha uzalishaji  ni jambo muhimu la kuhakikishja kwamba keki ya kitaifa inamfikia kila mmoja  ili kuboresha  hali ya maisha ya kila mkenya ,hakuna kingine kitakachofaulu’ Odinga amesema kupitia taarifa .

“ Kiwango cha keki ya kitaifa kimekuwa kikipungua kila mwaka  ilhali idadi ya watu wanaoingoja imekuwa ikiongezeka .Ndio kwa sababu kugawana shilingi bilioni 316 kw akaunti 47 ni tisho kwa uthabiti wan chi yetu  na umoja.’

Raila amesema  magavana wanafaa kuhakikisha kwamba kuna uzalishaji wa kutosha katika kaunti .

“ Tunafaa kuona ushirikiano wa vitengo vyote viwili vya serikali kutathmini masuala kama ya kodi ili  hatua hiyo iweze kuvutia uwekezaji na biashara  na sio kuzuia ukuaji huo hasa katika maeneo ya mashinani’

Raila  pia amelalamikia alichotaja kama kutengwa kwa wakulima  wadogo wadgo ambao huchangia ustawi wa  uchumi wa maeneo ya mashinani .