Sina uhusiano na Diamond, Zuchu asema

Zuchu na Diamond
Zuchu na Diamond
Taarifa ya Elizabeth Ngigi

Mwanamuziki wa lebo ya Wasafi  Zuchu amezungumzia uvumi unaozingira taaluma yake na ngoma yake mpya na boss wake Diamond Platnumz.

Zuchu alisajiliwa na lebo ya Wasafi inayomilikiwa na Diamond mwaka huu na amejipata katika njia panda huku jina lake likitamba kwa mambo mengine maovu.

Katika mahojiano na Wasafi Media, Zuchu alikanusha uvumi kwamba amekuwa akilala na boss wake na hiyo ndio sababu Diamond aliachana na Tanasha Donna.

Alisema kwamba uhusiano wake na Diamond ni wa kikazi na akiwa nje ya studio Diamond anakuwa ndugu yake mkubwa. "Hatujawahi kuwa katika mapenzi".

"Ukaribu wangu na boss wangu Diamond Platnumz ni kwa ajili ya kazi, anatumia muda mwingi kunipromote," alisema.

"Hajawahi hata kunionyesha dalili za kunitaka, ni kama kakangu. Ni ngumu sana kucheza vile na mtu ambae unamuheshimu. Lakini nashukuru Boss Sallam SK alisaidia kunifanya niwe comfortable."

Zuchu ametoa nyimbo kadhaa na Diamond, ukiwemo 'Cheche' ambao umeondolewa kutoka Youtube kutokana na maswala ya umiliki.

Tanasha likuwa amedai kwamba Zuchu aliiba mistari yake.

Zuchu hata hivyo, alisema kwamba alifanya wimbo huo kwa lugha ya Kihispania ili asijipate katika njia panda na Tanasha lakini bado amejipata katika hali hiyo.

“Idea ya kuimba kihispania ilikuja baada ya kusikiliza beat la wimbo wa 'Cheche'. Sikumuiga Tanasha,” alisema.