Ukiachana na mtu ,achana naye kwa uzuri+Podi ya Yusuf Juma

thursday
thursday
Kuna makovu ambayo baadhi ya watu huyabeba wanapotengana na mtu katika mahusiano au ndoa .Wasichojua ni kwamba makovu hayo huweza kukuvuta nyuma na kukuzuia kupiga hatua kwenda mbele .

   Katika podi hii ,leo tunakueleza jinsi unavyofaa kupiga hatua kwenda mbele na maisha yako hata wakati uhusiano wako na  mtu unapofika tamati.Sio lazima umtakie mabaya mpenzi wako wa zamani au utake kuyafutialia maisha yake baada ya uhusiano wenu kuisha .

 Kuachana na mtu ni fursa kwako kujijua na kufahamu unachotaka .Pia ni wakati wako kuduruhusu matarajio yako katika uhusiano mwingine katika siku za usoni .