Je Wazazi wako tayari kuwaachilia wanao kurudi shuleni?+Podi ya Yusuf Juma

Walimu kuanzia leo wanaripoti shuleni kabla ya  serikali kutangaza siku ambayo wanafunzi wataanza kurejea shuleni tangu kufungwa kwa shule katikati ya mwezi machi kwa ajili ya janga la corona .

 Hata hivyo wazazi wengi wamelalamikia hatua ya kukanganywa na wizara ya elimu ambayo hapo awali ilisema shule zingefunguliwa mwaka ujao .wengi wanasema hawana fedha za kuwalipia wanao karo za shukle iwapo serikali itazifungua shule  wakati wowote kabla ya januari mwaka  ujao . katika podi hii tunaeleeza shauku na kero za wazazi ,walimu na  matayarisho ya kufunguliwa kwa shule