Patanisho:Mume wangu amekuwa akiwaambia wanangu nina wanaume wengi

Bwana Shem,35, kutoka Kawangware alituma ujumbe ili apatanishwe na mke wake Moraa,27, ambaye walikosana naye mwezi jana,huku akisimulia masaibu yake alisema kuwa alimpata na watoto wawili huku naye akiwa na watoto huku nje.
"MImi na mke wangu ni watu wa hasira, tulikosana na mke wangu baada ya kusema kuwa nina mchunga sana hii ni baada ya kumpata anapigiwa simu na watu

alienda tu hapa Kawangware kwa mama yake, nimeenda mpaka kwao mwishowe mama yake aliniambia napaswa kuzungumza naye ninapozungumza naye ananiambia kuwa siwezi badilika

nilipokuwa namuoa alikuwa na watoto wawili, niliona ndoa yetu itakuwa kamili kwa maana hata mimi nina watoto nje." Alieleza Bwana Shem.

Moraa kwa upande wake alisema kuwa hataki kurudiana naye, huku akieleza alisema,

"Nilikuwa nikipigiwa simu ata kama sijui huyo mtu Shem ananigombanisha sidhani kama ni wivu kwa maana nikipigiwa na mama yangu alikuwa ananiambia heri singekuwa na mama

Nadhani mume wangu alikuja kugundua kuwa ananipenda baadaye lakini si mara ya kwanza ambapo alikuwa ananitaka kwa maana nilimpenda sana

Alikuwa pia anaambia watoto wangu kuwa yeye si baba yao na hata kuwaambia kuwa mimi nina wanaume wengi,ilifika mahali nikajiuliza kama mimi ndio mwanamume kwa uhusiano wetu."

Moraa alisimama na msimamo wake na kusema kuwa hayuko tayari kurudiana na Shem.