Victor Wanyama akana madai alifanya ngono na mwanasosholaiti Shakillah

Kapteni wa timu ya mpira wa kandanda Harambee stars Victor Wanyama ametoa tangazo huku akikana kuwa anamfahamu wala kuwa na uhusiano na mwanasosholaiti Shakillah.

Hii ni baada ya ya video ya Shakillah kuenea sana kwenye mitandao ya kijamii huku akidai kwamba amefanya ngono na baadhi ya wanaume mashuhuri wa humu nchini miongoni mwao akiwa ni Wanyama.

https://twitter.com/VictorWanyama/status/1310872610721468421

Katika tangazo lake alisema kuwa hamfahamu wala kumjue mwanasosholaiti huyo ambaye yuko katika video hiyo na kusema madai hayo.

"Umakini wangu umeletwa katika video ambayo imesambaa sana kwenye mitandao ya kijamii, huku ikiwa na madai ya uongo na uzushi ambao haja yake ni kuleta jina langu kwenye kashfa na kuniharibia sifa

natamani kujitenga na na video na usemi ulio katika video hiyo ya kukashifu,madai ambayo yamefanyika katika video hiyo na ya uzushi na sura bora ya mtengenezaji

Sijawahi patana na mtu yeyote ambaye yuko katika video hiyo, na laani vikali wote mwanamke mwenye yuko katika video hiyo na mchapishaji video Arthur Mandela na kupitia mtandao wake wa kijamii wa instagram  @Xtiandela kwa kuhimiza utengano wa  mtu mmoja ambaye alisema madai ya uongo." Ulisoma ujumbe wake Wanyama.

Wanyama alisema kuwa walitaka kupata wafuasi wengi wa habari yao kupitia video hiyo bali ameagiza timu yake kufuata tiba zote za kisheria zitakazopatikana.

Mwanasosholaiti kupitia video hiyo alisema ya kwamba baadhi ya wanaume aliofanya ngono nao na kumlipa ni Willy Paul,Masauti,Brown Mauzo.Khaligraph Jones miongoni mwa wingine.