PATANISHO:Mke wangu wangu alienda baada ya kunifumania na mpango wa kando

Bwana Libese alituma ujumbe apatanishwe na mke wake,Mary ambaye walikosana miezi michache iliopita baada ya kumpata na mpango wa kando.
"Tulioana na mke wangu mwaka wa 2011, tumebarikiwa na watoto wanne,mke wangu alinipata nikitaka kumuingiza mpango wangu wa kando

nimemuoma msamaha lakini amekataa, alienda kuodisha nyumbani mahali pengine,nilikuwa na mpango wa kando kwa maana mke wangu hajaweza kunitosheleza haki yangu

amekuwa akifanya kazi mpaka usiku anaingia kitandani saa nane usiku wakati ambao nataka kuamka na kuenda kutafuta kibarua."Libese aliongea

Lakini kwa kawaida kuna kitu ametuficha? haya basi wacha tuone vile mkewe alikuwa na ya kusema.

"Nimeishi na Libese tangu akiwa shule lakini kazi yake ni kuingia na kutoka si fahamu pesa zake vile anazitumia ni mimi nang'ang'ana na kufanya mahitaji yote

mbali na hayo amekuwa na mipango ya kando nyingi, analeta mwanamke mmoja baada ya mwingine wana lala naye kwa kitanda yetu

Mimi nikifanya makosa wazazi wake wananiita malaya akifanya makosa hawaoni makosa yake bali wananiekelea makosa yote,nimeishi naye huku akishinda kila wakati kusema atabadilisha tabia yake lakini hajabadilisha

mimi nahofia wanangu sitaki kuwaacha wangali wachanga kwa maana humu nje huwezi jua wala kufahamu mtu ambaye ana ugonjwa na hana."