Unafaa kujitayarisha vipi kwa uwezekano wa kupoteza kazi yako?+Podi ya Yusuf Juma

Kupoteza kazi sio jambo ambalo mtu anaweza kulitamani lakini sasa baada ya kuibuka kwa janga la corona ,watu wengi walipoteza kazi zao na kipato.Pana mjadala sasa kuhusu iwapo ni bora kuanza kujitayarisha kwa uwezekano wowowte wa kukatika kwa kipato chako kwa ajili ya kukosa ajira .

Watu wengi hupatwa kighafla na janga hilo la kupoteza kazi na wataalam wanasema pindi unapopata kazi ,unafaa kuanza kujitarayrisha kwa siku ambayo kazi hiyo tafika mwisho .Kuanzia kuweka akiba hadi kujishughulisha na vyenzo vingine kwa kupata kipato -njia za kupunguza mshutuko na msonono unaotokana na kupoteza kazi ni nyingi na tumezijadili katika Podi hii

Ripoti mpya ya shirikisho la waajiri nchini FKE imeonyesha kwamba  virusi vua corona vilisababisha kupotea kwa asilimia 80 ya kazi katika sekta ya kibinafsi tangu mwaka wa 2015

Matokeo ya utafiti huo yaliyotolewa wiki jana yanaonyesha kwamba  jumla ya idadi ya wafanyikazi waliopungua katika kampuni zilizohojiwa ilipungua kutoka 406 hadi 372 ,upungufu wa asilimia 8.3 wa jumla ya idadi ya wafanyikazi .Akiitoa ripoti hiyo ,afisa mkuu mtendaji wa FKE  Jacqueline Mugo   amesema uchunguzi uligundua kwamba kulikuwa na matatizo ya  uhaba wa fedha ,opareshenu na msururu wa usambazaji wa bidhaa na huduma uliathiriwa sana na janga la covid 19 .