Baraza la mawaziri wa Jumuiya ya afrika mashariki limeunga moono jitihada za waziri wa spotai Amina Mohammed kuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la biashara WTO
Baraza hilo kupitia taarifa siku ya jumatatu kuimwidhinisha Amina ni azimio linaoambatana na msimamo wa rais wa Rwnada Paul Kagame ambaye ndiye mwenyekiti wa baraza la marais wa Jumuiya ya Afrika mashariki anliyependekeza kwamba EAC imuunge mkono Amina kuipata kazi hiyo .
Taarifa hiyo imesema balozi Amina Mohammed ameidhinishwa kama mgombeaji wa EAC kwa nafasi hiyo .
Wiki jana mshikilizi wa dunia wa rekodi yam bio za Marathon Eliud Kipchoge alimuidhinisha Amina kwa kazi hiyo .
Katika ujumbe wake wa kumuidhinisha , Kipchoge alisema Amina ameonyesha weledi wa kufaulu hata katika hali ngumu .