Jaji John Onyiego amesitisha kesi hiyo siku a jumatatu baada ya Ojaamong kuwasilisha ombi akiwashtumu mashahidi wa upande wa mashtaka wa kumtishia .
Kesi hiyo imesitishwa hadi oktoba tarehe 12 ambapo mahakama itatoa maelekezo Zaidi .
Ojaamong kupitia wakili wake James Orengo analishtumu kundi la mashtaka likiongozwa na Taib Ali Taib kwa kuvuruga ushahidi na kuwatishia mashahidi wake .
Gavana huyo alifikishwa kortini mwaka wa 2018 kwa kutumia vibaya maamlaka ya afisi yake na mashtaka mengine kuhusiana na ufisadi .
Anashtumiwa wa kusaini makubaliano na Madam R Enterprises Ltd katika mradi wa ukusanyaji taka bila kuzingatia sheria za usimamizi wa raslimali za umma na kusababisha kupotea shilingi milioni 8 pesa za umma . ameshtakiwa pamoja na Madam R na maafisa wengine wa kaunti
Upande wa mashtaka umewaita mashahidi 20 na kufunga kesi yake februari tarehe 20 mwaka huu .