Patanisho:Mume wangu alinioa licha yake kujua ana mke nyumbani

Leo katika kitengo cha patanisho bwana Sam Edward alituma ujumbe apatanishwe na mke wake ambaye walikosana naye wiki tatu zilizopita baada ya kugundua kuwa ana mke mwingine nyumbani.
"Mimi na mke wangu Salome tumebarikiwa na watoto,4, mke wangu wa kwanza aliaga dunia na kuniacha na watoto wawili na kumpata Salome na wengine wawili

Nikiwa na mke wangu wa kwanza alienda kwao na kuoa mke mwingine na huyo akabarikiwa na mtoto mmoja, mke wanguu wa kwanza aliporudi nyumbani huyo mwingine alienda kwao

mke wangu aliaga dunia na kuoa mke mwingine, baada ya kumuoa yule mwingine alirudi baada ya kusikia kuwa nimeoa, mke wangu alienda kwa sababu hiyo na pia alisema kuwa nabugia pombe sana ilhali nabugia kidogo." Alieleza Bwana Edward.

Kwa kawaida lazima mtu afiche makosa yake, lakini swali ni je kuna kitu chochote ametuficha baada ya kueleza haya? haya basi mkewe Salome alikuwa na haya ya kusema.

"Nilipokuwa napelekwa nyumbani nilifika na kumpata huyo bibi mwingine nyumbani, alikuwa anaishi huko nilipomuuliza bwana Edward aliniambia kuwa alirudi alipofahamu nami naenda nyumbani

tena akipata pesa anakunywa pombe na hata kunichapa na kunitusi matusi mabaya, mimi nimechoka,pia ni muongo ana mwanamke mwingine pia ambaye anasema walikuwa katika uhusiano." Alisema Salome.

Ni ushauri upi unaweza kumpa bwana huyo licha ya kuwa na bibi nyumbani bali anamtaka Salome?