'Wewe ni nguzo ya kushangaza katika familia,'Mtangazaji Jalang'o amsifia mkewe

Mcheshi na mtangazaji Jalang'o hii lei amesherehekea kuzaliwa kwa mke wake hii leo,mmcheshi huyo alipakia picha ya mkewe kwenye mtandao wake wa kijamii wa instagram na kumpa sifa tele.

Hii leo ni siku maalum ya mkewe Jalang'o na baada ya kuposti picha yake basi aliandika ujumbe mfupi akimsifia kwa kuwa nguzo ya kushangaza katika maisha yake.

"Leo ni siku yako, happybirthay mpenzi wangu, asante kwa kuwa mtu wa kushangaza wewe ni nguzo ya kushangza ambayo iko katika familia yetu

wacha ukurasa huu mpya ukafungua malango yako happy birthday mpenzi jaber ni jaber." Aliandika Jalang'o.

https://www.instagram.com/p/CF6NFlrn8sC/

Baada ya posti yake watu mashuhuri marafiki,watangazaji na hata mashabiki walimtakia mkewe mcheshi huyo siku njema ya kuzaliwa.

Mcheshi huyo anapenda kutumia wakati wake na mpenzi wake huku awali akimpeleka matembezi Malindi.