Samido akana kuwa na uhusiano na Karen Nyamu, ni rafiki tu

Muhtasari

• Samido alisema kwamba taarifa iliyochapisihwa ni ya uongo na kwamba wao ni marafiki tu.

• Nilikuwa nahofia mke wangu lakini tusha zungumza na yuko sawa. Anajua siko katika uhusiano na Karen

Mwanamuziki wa benga Samido
Mwanamuziki wa benga Samido
Image: HISANI

Taarifa ya Elizabeth Ngigi

Mwanamuziki wa mitindo ya benga Samido amejibu madai kwamba ana uhusiana wa kimapenzi na mwanasiasa Karen Nyamu, wakili na mkurugenzi wa kampuni ya maji ya Nairobi.

Akizungumza na Word is, Samido alisema kwamba taarifa iliyochapisihwa ni ya uongo na kwamba wao ni marafiki tu.

 

"Nina mke na watoto na sina mipango wa kuanzisha familia nyinge wakati huu mgumu wa kiuchumi," alisema.

"Sijakuwa na uhusiano wa kimapenzi na yeye, amekuwa tu shabiki wangu kwa muda mrefu."

Mwanamuziki huyo aliyeimba wimbo wa 'Mumbi' anasema kwamba habari hizo zimemshangaza sana kwa sababu hakuwa hata Nairobi wikendi."

"Hata sijakutana naye kwa zaidi ya miezi mitatu baada ya kusitisha urafiki wetu nilipogundua kwamba ungevuruga familia yangu " alisema.

Alipoulizwa kuhusu vile mke wake alichukulia babari hizi, Samido alisema yuko sawa.

"Nilikuwa nahofia mke wangu lakini tusha zungumza na yuko sawa. Anajua siko katika uhusiano na Karen ."

Wakati Word Is walipojaribu kuzungumza na Karen Nyamu, alidinda kuzungumzia uja uzito wake na kama ana beba mtoto wa mwanamuziki huyo.

 

"Sijui nani alimpa habari mwanablogi huyo lakini sitaki kuzungumzia jambo hili."

Karen alijulikana sana mwaka 2017 alipowania wadhifa wa mwakilishi wadi wa kaunti ya Nairobi.

Anatarajia mtoto wa pili.