Magufuli awaambia watanzania kuombea Kenya

Muhtasari

• Aliwaambia watanzania kwamba kama tu vile walimuomba Mungu kuwaondolea Corona, wakati umewadia kwa wao kujiunga na wakenya kuombea Kenya.

• Rais Kenyatta alitangaza kuwa Kenya itaandaa .maombi ya siku tatu kuanzia Ijumaa hadi Jumapili.

• Rais Kenyatta alitangaza kuwa Kenya itaandaa .maombi ya siku tatu kuanzia Ijumaa hadi Jumapili.

 

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amewataka watanzania kutenga muda na kujiunga na wakenya kuombea janga la virusi vya corona.

Magufuli siku ya Ijumaa aliwaambia watanzania kwamba kama tu vile walimuomba Mungu kuwaondolea Corona, wakati umewadia kwa wao kujiunga na wakenya ambao wana uhusiano wa karibu nao kuomba pamoja.

Magufuli alikuwa akizungumza katika mkutano wa kampeini wa chama cha Mapinduzi katika uwanja  wa Benjamin Mukapa mjini Dar es Salaam.

"Miezi michache iliyopita nchi yetu ilikuwa miongoni mwa zile zilizokuwa zimeathirika na Coronavirus, tuliketi na viongozi wa kidini na kuomba Mungu ailinde nchi yetu. Twamshukuru Mungu kwa sababu kwake hakuna jambo gumu alitusaidia kushinda ugonjwa," Magufuli alisema.

"Leo asubuhi kabla nije hapa nimesemezana na mwenzangu na rafikiki wetu rais Uhuru Kenyatta wa Kenya. Ameamua naye pia katika kipindi cha siku tatu kuanzia leo hadi Jumapili kumuomba Mungu ili ugonjwa wa korona uondoke Kenya. Nawaomba sana watanzania wenzangu tushirikiane na wenzetu wa Kenya kwenye maombi hayo ili ugonjwa huo uwaondokee," aliongeza.

Magufuli alisema kwamba ana uhakika kuwa Mungu aliyewasaidia, anasikia, hujibu maombi na hataangusha Kenya.

Rais Kenyatta alitangaza kuwa Kenya itaandaa .maombi ya siku tatu kuanzia Ijumaa hadi Jumapili.

Siku ya Jumamosi rais ataongoza maombi ya pamoja katika Ikulu Nairobi kuanzia saa nne mchana.