Nimebarikiwa kukuita Malkia wnagu-DJ Mo

‘Wewe ni wangu hadi kifo’ DJ Mo amuambia mkewe Size 8

Wawili hao waliadhimisha miaka 7 ya ndoa siku ya jumapili

Muhtasari

 

  •  Ndoa yao imekumbwa na msukosuko baada ya Mwanamke mmoja kufichua kwamba ana uhusiano na DJ Mo
  •  Size 8 amesema kwamba atazidi kuiombea ndoa yake na Mo 

 

DJ Mo na Size 8

Ndoa ya msaniia wa gaospel Size 8 na DJ Mo imekuwa katika ndimi za wengi na hasa ktika mitandao ya kijamii.Lakini yaonekana ‘The Murayas’ kama wanavyipenda kujitambulisha hawana  mda wa kusikiza upondaji na cheche za hapa na pale kuhusu maisha yao ya ndoa .

 Katika  posti moja ya instagram ili kusherehekea miaka saba ya kuwa pamoja ,DJ Mo ameamua kufunguka roho na kubwaga kila kilicho moyoni mwake huku akiahidi kuwa na mke wake hadi kifo !

Hakuna kitakachobadilika hadi kifo. Mama ya watoto wangu na msingi wa familia yangu….’ Sehemu ya ujumbe huo inasoma

 DJ Mo ameendelea kuafoka mistari mitamu akisema ;

 ‘Tumepitia panda shuka nyingi lakini tumesalia pamoja  ,unajua siogoipi changa moto na hili pia silikimbii . Nimebarikiwa kukuita Malkia wangu  licha ya kuwa na vikwazo vingi’

  Ujumbe huo ni dhahiri kwamba DJ Mo yuko tayari kuendelea kujenga uhusiano mzuri na Size 8 licha ya kuibka madai kwamba alikuwa na mwanamke wa pembeni .Wengi walijitokeza kumpiga jeki DJ Mo wakati alipotundika ujumbe huo katika instagram huku msanii Akothee  akitoa maoni chini ya posti hiyo akiwapa heko na pia kuwahimiza waipiganie ndoa yao.msanii mwingine Wahu pia alioandika ujumbe wa kuwahongera kwa miaka saba ya ndoa