Watu kumi waaga dunia kutokana na corona
318 wapatikana na virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya 41,937
215 ni wanaume huku 103wakiwa ni wanawake
Kenya hii imerekodi visa 318 vipya vya maambukizi ya corona na kufikisha idadi jumla ya 41,937 hii ni kutokana na sampuli 2, 592 zilizopimwa katika saa 24 zilizopita.
Vile vile katibu msimamizi wa afya Rashid Aman amesema kuwa watu,10, wameaga dunia kutokana na virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya 787 walioaga dunia kutokana na virusi hivyo.
Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 215 ni wanaume huku 103 wakiwa ni wanawake, huku hayo yakijiri watu 243 wamepona corona na kufikisha idadi jumla ya 31,340 a watu waliopona virusi hivyo,
Pia akati ya maambukizi hayo mgonjwa wa umri wa chini ana miaka mitatu huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 90.