Mlipuko wa corona:Watu,602 wapatikana na corona

Muhtasari
  • Watu 602 wapatikana na virusi vya corona huku 8 wakipoteza maisha yao
  • Hii ni baada ya sampuli 5,618 kupimwa saa 24 zilizopita
kagwe
kagwe

kenya hii leo imesajili visa 602 vipya vya maambukizi ya corona na kufikisha idadi jumla ya 43,143 watu walioambukizwa corona hii ni baada ya sampuli 5,618 kupimwa saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 585 ni wakenya huku 17 wakiwa raia wa kigeni, 401 ni wanaume na 195 ni wanawake.

Mgonjwa wa umri wa chini ana mwaka mmoja huku mwenye umri wa juu zaidi akiwa na miaka 93.

Vile vile watu 80 wamepona virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya 31,508 huku 51 wakipona wakipokea matibabu ya nyumbani huku 29 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti humu nchini.

Huku hayo yakijiri watu 8 wameaga dunia kutokana na virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya watu 805 walioaga kutokana na corona.