Gavana Hassan Joho atupilia mbali ripoti kwamba amejiuzulu kama naibu mwenyekiti wa chama cha ODM

joho
joho

Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho ametupilia mbali habari za barua inayoenea kwenye mitandao ya kijamii ya kwamba amejiuzulu kama naibu mwenye kiti wa chama cha ODM.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook Joho alisema ya kwamba chama hicho kiko imara kama awali.

Kupitia barua hiyo Joho alikuwa ameuliza uongozi wa chama hicho kuwapa vijana nafasi ya kuwa viongozi wa chama hicho na kusikiza maoni yao.

 

"Nachukua fursa hii kuwashukuru kwa nafasi ambayo mlinipa kama chama kufanya kazi kama naibu mwenyekiti wa chama hiki

naamini nilipokuwa nafanya kazi nilifanya vyema pamoja na wanachama, ikiwemo kupanga kampeni eneo tofauti humu nchini hata mapishi licha ya ugumu wa pesa tuliopitia." Barua ilisoma.

Ni barua ambayo ilikuwa imeandikiwa kinara wa chama hicho huku akisema ya kwamba kuwa naibu kumekuwa somo kwake na kuwa amesoma mengi.

 

Joho alisema kuwa hizo ni habari bandia na kuwa chama kiko imara, pia chama cha ODM kilitupilia mbali ripoti hizo na kusema kuwa habari hizo ni za uongo.