Poleni sana:Boni Khalwale aomboleza kifo cha ng'ombe bingwa wa mapigano ya ng'ombe

Muhtasari
  • Mchezo wa mapigano ya ng'ombe unapaswa kutambuliwa kama moja wapo ya michezo humi nchini
  • Pogba ameaga dunia kutokana na homa
khalwale
khalwale

Aliyekuwa seneta wa kaunti ya Kakamega Boni Khalwale amemuomboleza ng'ombe anayefahamika kama Pogba hii ni baada ya ng'ombe huyo kuaga dunia kutokana na home, na ambaye amekuwa akishiriki mapigano ya ng'ombe katika kaunti hiyo.

Wapenzi na mashabiki wa mchezo huo wamo katika mshtuko mkubwa kufuatia kifo cha ng'ombe huyo.

Pogba alichukua utawala kutoka kwa mwendazake Iminyi, ng'ombe huyo alipigana na ng'ombe hao wengine na kuwa mshindi mnamo mwaka wa 2016 Desemba mchezo uliokuwa umeandaliwa katika kijiji cha Malinya.

 

Kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter Boni alitangaza kifo cha ng'ombe huyo huku akisema kuwa mapigano ya ng'ombe yanapaswa kuteuliwa kuwa moja wapo ya michezo humu nchini.

"Malinya Pogba ameaga, ameenda kupumzika na iminyi the G.O.A.T ameaga dunia kutokana na homa ya pwani ya mashariki

Aishi kwa muda mrefu mfalme wa mchezo huu mzuri." Aliandika Khalwale.

Kupitia kwa posti nyingine Khalwale alimuomboleza ng'ombe huyo kwa ujumbe huu huku akisema ni pigo kubwa kwa mashabiki wa mchezo huo.

"Habari za kuhuzunisha kutoka Malinya asubuhi hii ya leo, Pogba ameaga dunia hii ni pigo kubwa, pole sa @KBonimtetezi mapigano ya ng'ombe yanapaswa kutambulika kama moja wapo ya michezo humu nchini."