DP Ruto uliahidi vijana wetu kompyuta lakini ukawaletea mikokoteni-Babu Owino

Muhtasari
  • Hakukua na ndoa kati ya William Ruto na Uhuru Kenyatta ilikuwa ndoa ya kuja tuishi pamoja
  • Ruto aliahidi vijana kompyuta badala yake aliwaletea mikokoteni babu owino asema
  • Ruto anapaswa kufahamu tunahitaki kiongozi wa kisiasa na wala si mfanyabiashara wa kisiasa
  • Hakuna mzazi atafurahi mtoto wake akisukuma mkokoteni
babu.owino (1)
babu.owino (1)

Mbunge wa Embakasi Mashariki Paul Ongili almaarufu Babu Owino amezungumzia uhusiano uliopo kati ya rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto.

Pia mbunge huyo alizungumzia vile naibu aliwaahidi vijana kuwaletea kompyuta ndogo badala yake akawaletea mikokoteni huku akituia jina la 'hustler'.

Huku kwa utani alisema kuwa hakukuwa ndoa yeyote kati ya naibu Ruto na Uhuru Kenyatta bali ilikuwa tu uhusiano wa kuishi pamoja au ukienda 'come we stay'.

 

Huku akizungumza haya siku ya JUmamosi akiwa katika eneo bunge la Saboti alimkashifu naibu Ruto huku akisema anawasaidia vijana na mikokoteni baada ya serikali aliofanyia kazi kukosa kutimiza ahadi zao kwa kuleta kazi kwa vijana.

"Dunia yote inataka kusikia haya bwana Ruto kati yako na Uhuru hakukuwa na ndoa yeyote, ilikuwa tu kuja tukae pamoja (come we stay)

Ndugu yangu Ruto uliahidi vijana wetu kompyuta ndogo lakini badala yake ukawaletea mikokoteni

Uliahidi kujenga stadia kadhaa lakini unaleta mikokoteni ,nani anataka mtoto wake akuwe anazunguka hapa na pale akivuta mikokoteni." Alizungumza Babu Owino.

Pia mbunge huyo aisema kwamba Ruto anapaswa kujua kuwa wanahitaji viongozi wa siasa na wala si wafanyabiashara wa kisiasa.

Babu alikuwa amehudhuria sherehe ya mbunge wa eneo hilo Caleb Hamisi.

"Ruto anapaswa kujua tunataka kiongozi kiasiasa na wala si mfanyabiashara wa kisiasa, tunahitaji mtu ambaye atamsaidia Uhuru Kenyatta kupanga serikali."