DCI yamtia mbaroni mshukiwa aliyetekeleza unajisi,mauaji na ubakaji Ruiru

Muhtasari
  • Maafisa wa DCI wamtia mbaroni mshukiwa wa ubakaji mauaji na unajisi ruiru
  • Mshukiwa huyo alitekeleza kitendo hicho mnamo tarehe 16 Oktoba mwaka huu
  • Maafisa hao walitumia kamera za siri kuchunguza kisa hicho
Pingu
Image: Radio Jambo

Maafisa wa polisi wa DCI asubuhi ya Jumanne,20,wamemtia mbaroni mshukiwa mmoja aliyetekeleza ubakaji, unajisi na mauaji eneo la Ruiru.

Levy Abubakara,36 alitekeleza kitendo hicho mnamo mwezi wa Oktoba ,16,2020 huku akiwa na wenzake wawili katika eneo la Membley kata ndogo ya Ruiru.

Levy alikamatwa baada ya maafisa hao kuchunguza kamera za siri ili kuchunguza kesi hiyo, mshukiwa huyo alionekana na wenzake wakiingia nyumbani humo na kumnajisi msichana wa miaka 16, na kisha wakambaka mfanyakazi kabla ya kumuua.

 

Washukiwa hao waliwafunga wawili hao na kamba na kisha wakamuua mfanyakazi huyo, washukiwa hao wamo mikononi mwa polisi huku wakingoja kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yao.