Shujaa wako ni nani? Wakenya washerehekea mashujaa wao kwa jumbe hizi

Muhtasari
  • Siku ya mashujaa huku kapteni Daudi akisheherekewa kama mmoja wa mashujaa
  • Daudi aliwaokoa wakenya kutoka nchi ya New York City wakati wa janga la corona
20200404_114303
20200404_114303

Leo hii ikiwa ni siku ya kusheherekea mashujaa tofauti wa humu nchini na mashujaa ya mwaka wa 57 tangu nchi ya kenya kupata uhuru wakenya wengi kupitia kwenye mitandao ya kijamii wameweza kuwatambua mashujaa wao, wanariadha,waigizaji,wasanii na wakenya wengi ambao walifanya jambo la ushujaa.

Je wamkumbuka kapteni Daudi Kimiyu ambaye aliwaokoa wakenya wengi wakati wa janga la corona na kuwaleta humu nchini licha ya janga hilo kuwa kali mno?

Wakenya wengi wameweza kumsheherekea kapteni huyo ambaye baada ya kuwaokoa wakenya hao kutoka nchi ya new york city kisha akaambukizwa virusi hivyo mwishowe akafariki.

Huu hapa ujumbe wa kumpongeza mwendazake,

"Wakati New York City ilikuwa katika lockdown, na mkumbuka kapteni Daudi Kimuyu kibati aliwasaidia wananchi wa kenya ambao walikuwa wamekwama nchini humo

Kapteni huyo alilipa gharama ya kuwa shujaa, wewe ni shujaa wangu." Ujumbe Ulisoma.

Kwa kweli hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kosa shujaa wake, wewe kama Mkenya shujaa wako ni nani na kwa nini unamsheherekea kama shujaa?

Mungu azidi kuilaza roho yake Daudi mahali pema peponi.