Muhtasari
- 12 waaga dunia kwa ajili ya corona
- watu 1,068 waambukizwa corona
Watu 1,068 wamepatikana na virusi vya corona baada ya sampuli 7,556 kupimwa katika saa24 zilziopita na kufikisha jumla ya visa hivyo nchini hadfi kufikia sasa kuwa 47,212.
Kutoka visa hivyo 1,044 ni wakenya ilhali 24 ni aia wa kigeni . wanaume ni 666 ilhali wanawake ni 402 .Mgonjwa wa umri wa chini ni mtoto wa miezi sita ilhali wa umri wa juu ana miaka 96 .
Leo watu 290 wamepona na kufikisha 33,050 idadi ya waliopona corona
Watu 12 wameaga dunia leo na kufikisha 870 jumla ya walioangamizwa na ugonjwa huo nchini .