COVID-19: Watu 12 waaga, visa 947 vipya vyaripotiwa

Mutahi Kagwe
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe Mutahi Kagwe

Siku ya Jumamosi wizara ya afya ilihibitisha visa 947 vipya vya virusi vya Corona kutoka sampuli 6,862 zilizookotwa katika masaa 24 iliyopita.

Hii inamaanisha idadi ya walioambukizwa imefikia 48,790 sasa.

Kupitia ujumbe uliotumwa na waziri wa afya Mutahi Kagwe, idadi ya vipimo vilivyofanywa nchini vimefikia 653,229.

 

Waziri pia amethibitisha kuwa watu 455 wamepona huku 343 wakiwa wagonjwa waliokuwa nyumbani na 112 wakiruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospitali mbali mbali nchini.

Kutokana na kesi hizo 924 ni wakenya huku 23 wakiwa wageni. 595 ni wanaume na 352 ni wa jinsia ya kike.

Kutokana na visa hivyo vipya, mgonjwa mchanga zaidi ana umri wa mwaka mmoja huku mgonjwa mkongwe akiwa na umri wa miaka 96.

Hata hivyo Kagwe alitangaza kuwa watu 12 waliaga dunia huku idadi ya waliofariki ikifikia 896.