PICHA: Mcheshi Ben 'Othuol' Maurice azikwa

mazishi ya Othuol
mazishi ya Othuol

Mcheshi Ben Maurice almaarufu Othuol Othuol amezikwa leo nyumbani kwao katika kaunti ya Siaya Alego Ndere katika kijiji cha Gogagi.

Othuol aliaga dunia mnamo tarehe 11 Oktoba 2020 katika hospitali ya Kenyatta alipokuwa anapokea matibabu.

Mwili wa mwendazake ulitolewa katika makafani ya Chiromo hapo jana asubuhi na kupelekwa katika maeneo ya Kenyan National Theatre kwa ibada ya wafu.

Sherehe ya mazishi ya mwendazake zilianza saa mbili asubuhi.

Waombolezaji wote walikuwa wameulizwa wazingatie kanuni za wizara ya afya ili kuthibiti kusambaa kwa virusi vya corona.

Mwenye kiti wa Comedians in Kenya Society Waudo aliwashukuru wacheshi,marafiki na kila mmoja ambaye alisimama nao wakati huu mgumu.

Tazama picha za  mazishi ya mwenda zake;