Rais wa Poland apatikana na virusi vya Corona

Rais wa Poland Andrzej Duda
Rais wa Poland Andrzej Duda

Rais wa Poland Andrzej Duda amepatikana na virusi vya corona lakini anajihisi vyema. Hii ni kulingana na waziri mkuu wa nchi hiyo  Blazej Spychalski.

"Hapo jana rais alipatikana na virusi vya Corona. Rais anaendelea vyema na tunawasiliana na idara husika za matibabu," Spychalski aliandika kwenye mtandao wake wa Twitter. 

(The president yesterday was tested for the presence of coronavirus. The result turned out to be positive. The president is fine. We are in constant contact with the relevant medical services)

Kuambukizwa kwa Duda mwenye umri wa miaka 48, kumejia wakati nchi hiyo imeripoti visa vingi vya Corona huku nchi ikiandikisha rekodi mpya ya visa 13,600 siku ya Ijumaa.

Kuanzia leo kunatarajiwa kuwa na  vizuizi zaidi vya kuzuia kuenea kwa virusi nchini Poland, pamoja na kufungwa kwa mikahawa na baa kwa wiki mbili.

Wizara ya Afya iliripoti vifo 153 vya coronavirus siku ya Ijumaa, huku idadi ya walioambukizwa ikifikia  4,172

(Inaripotiwa na Marcin Goclowski Kuhaririwa na Jason Neely na Frances Kerry)