Wafungwa watatu waaga dunia, 1700 waambukizwa Corona

Kamiti
Kamiti

Zaidi ya wafungwa 1,700 wameambukizwa virusi vya corona. Dkt Azenga Kisivuli anasema wafungwa watatu wamefariki kutokana na virusi hivyo.

Kamishna mkuu wa idara ya magereza Wycliffe Ogalo amesema ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona katika magereza linatokana na ugumu wa kuzingatia kanuni ya mtu kukaa umbali wa mita moja kutoka kwa mwenzake.

Mkurugenzi wa huduma za afya wa magereza Kisivuli Anzenga alisema kukaa katika magereza ni mbali zaidi ya uwezo licha ya kuachiliwa kwa wafungwa wengine kuangalia idadi.

"Magereza yetu yalibuniwa kuwa na uwezo wa kushikilia watu 30,000 lakini ina wafungwa 55,000. Baada ya Covid-19 na kukaguliwa na kuachiliwa kwa wafungwa wengine, wakaazi ni 46,000. Hiyo bado ni imeidi nambari iliyopendekezwa, "Kisivuli alisema.

Alisema kukosekana kwa maeneo na vifaa vya kujitenga pia na  uhaba wa wafanyikazi wa matibabu ndani ya magereza kumeleta changamoto.

Ogallo alisema vifo vitatu vilivyosajiliwa ni pamoja na kifo cha mfanyikazi. Wote walikuwa na magonjwa  mengine kama Ukimwi, saratani na ugonjwa wa sukari.