Tetesi za soka duniani, Jumapili, Oktoba 25, 2020

Jorginho
Jorginho
Image: BBC

Kiungo wa kati wa Chelsea na Italia Jorginho, 28, amesema yuko "tayari kushauriana" na Arsenal na kukiri kuwa Gunners walionesha mpango wa kutaka kumnunua msimu huu wa joto. (ESPN Brazil - in Portuguese)

Mpango wa Real Madrid wa kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain Mfaransa Kylian Mbappe, 21, hautavurugika hata mkufunzi wa klabu hiyo Zinedine Zidane akiondoka. (AS)

Zidane anasisitiza "atakuwa na wachezaji hao hadi kufo" licha ya tetesi kuibuka kuhusu hatma ya Mfaransa huyo Real. (ESPN)

Tottenham Hotspur imempatia mshambuliaji wa Korea Kusini Son Heung-min kandarasi mpya ya miaka mitano ya thamani ya £200,000 kwa wiki pamoja na marupurupu mengine, ambayo ni karibu mara mbili ya marupurupu ya anayolipwa katika kandarasi ya sasa itakayomalizika mwaka 2023. (Football Insider)

Mkufunzi wa Spurs Jose Mourinho anamtarajia Son, 28, kutia saini mkataba huo mpya "hivi karibuni". (London Evening Standard)

Ajenti wa Mesut Ozil anadai kuwa mkufunzi wa Gunners Mikel Arteta hajakuwa mkweli kuhusu sababu ya kumuondoa mchezaji huyo waUjerumani katika kikosi chake. (Guardian)

Beki wa kushoto na nyuma wa Chelsea na Italia Emerson Palmieri, 26, huenda akaondoka Stamford Bridge mwezi Januari, huku Inter Milan, Roma na Napoli wakionesha dalili ya kuweka dao la kumnunua. (Sky Sports Italia, via Express)

Manchester City wanajiandaa kumsajili winga wa Partizan Filip Stevanovic kwa kima cha £6m mwezi Januari dirisha la uhamisho litakapofunguliwa. Kiungo huyo wa miaka 18- raia wa Serbia aliwahi kuhusishwa na Manchester United. (Manchester Evening News)

Paris St-Germain wanajiandaa kumpatia Neymar mkataba mpya endapo wataafikiana na mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil, 28. (Le10 Sport - in French)

Winga wa Everton na DR Congo Yannick Bolasie, 31, anawasaidia vijana chipukizi mjini Liverpool kupata mafunzo ya bure ya soka kipindi cha mapumziko. (Liverpool Echo)

Habari kutoka BBC