United na Chelsea wakabana koo, Liverpool yanyakua ushindi

Man U chelsea
Man U chelsea

Ligi ya Uingereza itaendelea hii leo huku  timu zikipiga mechi ya sita msimu huu. 

Hapo jana Manchester City walitoka sare ya bao moja kwa moja dhidi ya West Ham , huku Manchester United wakitoka sare tasa dhidi ya mahasidi wao  Chelsea.   

Mabingwa watetezi Liverpool nao walitua ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Sheffield United  ugani Anfield.  Southampton sasa  wanaalika  voingozi Everton, huku  Wolves ikikabana koo na Newcastle kabla ya  Arsenal kupimana nguvu na  Leicester City

Tottenham Hotspur imempatia mshambuliaji wa Korea Kusini Son Heung-min kandarasi mpya ya miaka mitano ya thamani ya pauni elfu 200,000 kwa wiki pamoja na marupurupu mengine, ambayo ni karibu mara mbili ya marupurupu ya anayolipwa katika kandarasi ya sasa itakayomalizika mwaka 2023.

Shirikisho la Soka nchini Uingereza FA limetishia kuzuia klabu za Uingereza kuwasajili wachezaji wa kimataifa kutoka nje ya Muungano wa Ulaya hadi pale Ligi Kuu zitakapo kubaliana kubuni sheria zinazowalinda wachezaji wa nyumbani baada ya Brexit.

 

Manchester City wanajiandaa kumsajili winga wa Partizan Filip Stevanovic kwa kima cha pauni millioni 6 mwezi Januari dirisha la uhamisho litakapofunguliwa. Kiungo huyo wa miaka 18- raia wa Serbia aliwahi kuhusishwa na Manchester United.