Jamaa aliyekuwa na mzozo wa ardhi na DP Ruto aaga dunia

Muhtasari
  • Adrian alikuwa na kesi ya mzozo wa ardhi na naibu rais William Ruto
  • Ruto aliagizwa na mahakama kumlipa mwendazake millioni 5 kwa kunyakua shamba lake
  • Adrian aliafa dunia mnmo tarehe,27 Oktoba 2020

Jamaa aliyeshinda kesi ya mzozo wa ardhi na naibu rais William Ruto aliaga dunia mnamo JUmanne,27,Oktoba.

Kifo chake Adrian Gilbert Muteshi, 86, kilitangazwa na gazetti moja la humu nchini huku wakiandika ujumbe huu.

"Ni kwa hali ya kina na ya huzuni kutangaza kifo chake Adrian aliyeaga dunia akiwa mjini Nairobi." Baadhi ya tangazo hilo ilisoma.

Tangazo hilo halikutangaza kiini cha kifo cha mwendazake, jamaa na marafiki wanatarajiwa kukutana kuanzia Alhamisi wiki hii mwendo wa saa kumi na moja hadi saa moja usiku katika eneo la United Kenya Club.

Adrian alitolewa shambani mwake Eldoret mnamo mwak wa 2007, wakati wa ghasia za uchaguzi, huku akimshtaki naibu rais kwa kuchukua shamba lake katika kaunti ya Uasin Gishu .

Kupitia kwa wakili wake, mahakama ya Nairobi ilitawala na kusema kuwa Adrian alipa korti ushahidi wa kutosha kuwa shamba hilo ni lake na pia kuthibitisha ni shamba lake huku Naibu rai akiagizwa kumplipa jamaa huyo millioni 5 kwa kunyakua shamba ya mwendazake.