PS wa elimu aripoti namba za wanafunzi na walimu walioambukizwa corona

Muhtasari
  • Tuache kuwalaumu watoto wetu ilhali wazazi hawazingatii kanuni za wizara ya afya
  • Wanafunzi 17 na walimu 33 waambukizwa corona nchini kenya
Belio Kipsang
Belio Kipsang

PS wa elimu Belio Kipsang mnamo JUmanne alitangaa na kuripoti wanafunzi 17 na walimu 33 ambao wamepata maambukizi ya virusi vya corona.

Kipsang alisema kuwa visa hivyo vimeripotiwa katika shule 35 ncchini kote.

Mwezi wa Oktoba kenya imekuwa ikirekodi visa vya juu zaidi huku wengi wakizidi kupoteza maisha yao.

 

Hata hivyo,Kipsang alisema kwamba maambukizi hayo hayana wasiwasi wowote kwa wizara ya afya na kwa ivyo hamna mpango wa kufunga mashule.

"Hatuna mipango ya kufunga shule labda tuagizwe na wizara ya afya, lakini tunafanya kazi pamoja ili kuangalia kama madarasa yale mengine yatafunguliwa." Alizungumza Kipsang.

PS kipsang pia alisema kuwa kidole cha lawama kitaelekezewa wazazi ambao wanahudhuria mikutano ya kisiasa.

"Changamoto yetu kubwa ni kwa wazazi ambao wanahudhuria kampeni za siasa na mikutano nyingine bila kuvalia maski tuache kuwalaumu watoto wetu

Kwanini mtuambie tuzingatie kutengana shuleni ilhali wazazi wetu wanahudhuria mikutano ya kisiasa bila ya kuzingatia jambo hilo."