'Gharama ya kutibu corona ni ghali sana,'Mbunge Githiaka asema huku akifichua haya

Muhtasari
  • Mbunge Githiaka adai alitumia milioni 3, kutibiwa corona

Mbunge wa Mukurweuni Anthony Githiaka amefichua kwamba hivi karibuni alikuwa ameambukizwa virusi vya corona.

Githiaka ambaye alikuwa akiongea katika Bunge la Kitaifa Jumanne, Novemba 17, aliwaambia wenzake matibabu ya COVID-19 yalimwacha amefilisika.

Mbunge huyo alifichua kuwa alitumia takriban KSh 3 milioni ambazo alisema ni pesa nyingi ambazo Mkenya wa kawaida hangeweza kupata kwa urahisi. 

 

"Gharama ya kutibu COVID-19 ni ghali sana. Kufikia wakati nilitakiwa kuondoka hospitalini, nilipewa bili ya takriban KSh milioni tatu. Nduguzanguni, ukiwa hapa Bungeni unaweza kufikiria kwamba una bimayaCOVID -19 lakini, wenyeji unaowawakilisha wanapoaga dunia, basi inamaanisha, wewe pia unapoteza kiti chako hapa." Aliongea Githiaka.

Maneno yake yanajiri siku chache baada ya mbunge wa Matungu Justus Murunga kuaga dunia kwa ajili ya maambukizi ya virusi hivyo.

Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa alielezea kusikitishwa na kifo cha Murunga, huku akimtaja kama "kiongozi mchapakazi na kiongooi shupavu."