Jamaa aliye mlawiti mtoto wa miaka 16 afungwa miaka 16

Dennis Okoth Onyango
Dennis Okoth Onyango
Image: corazon wafula

Haki imetolewa kwa mvulana wa miaka 16 ambaye alilawitiwa na jamaa kwa jina Dennis Okoth Onyango mnamo Oktoba 20, 2013.

Siku ya Alhamisi, hakimu mkuu wa Makadara, Heston Nyaga, alimhukumu Dennis Okoth Onyango kifungo cha miaka 15 gerezani.

"Kwa maoni yangu, mtuhumiwa hapaswi kuwa karibu na mtoto haswa mtoto wa kiume," hakimu aliamua.

Okoth alishtakiwa kwa kufanya kosa hilo katika mtaa wa Dandora phase IV katika Kaunti Ndogo ya Njiru, Nairobi.

Alikabiliwa pia na shtaka mbadala la kufanya kitendo kisichofaa na mtoto.

Okoth alikana mashtaka na upande wa mashtaka uliita mashahidi wanne kuthibitisha kesi yake.

Mdogo huyo alisimulia kuwa siku hiyo, alikuwa ameenda kutafuta makazi nyumbani kwa rafiki yake, baada ya kuwa na ugomvi na mama yake, Miriam Andusa, ambaye pia alimzaba kofi.

Rafikiye, Alude alikuwa anaishi na mshtakiwa.

Korti ilisikia kuwa usiku wa tukio kulikuwa na watu wengine watatu ndani ya nyumba hiyo.

Walitandaza kitanda sakafuni ambapo mtuhumiwa na mtoto mchanga walilala huku mvulana mwingine akilala na Allude kitandani.

Katikati ya usiku mwathiriwa alisikia Okoth akimpapasa kabla ya kuvuta suruali yake chini.

Mhasiriwa huyo alimkataza, lakini Okoth alimwambia akae kimya kwani kulikuwa na watu wengine chumbani hicho. Aliwacha kwa muda lakini baadaye ndipo alimlawiti.

Siku mbili baadaye, mtoto huyo mdogo alimuuliza rafiki yake Alude ikiwa mtuhumiwa alikuwa amemfanyia chochote, lakini hakumjibu na wala mlalamikaji hakumwambia kilichompata.

Alikwenda na kuripoti tukio hilo kwa mmoja wa walimu wake Samuel Karimi ambaye aliagiza apelekwe hospitali.

Kisa hicho kiliripotiwa kwa polisi baadaye.