'Sijui nilipata aje maambukizi ya corona ,'wakili Kipkorir aeleza jinsi alipigana na virusi hivyo

Muhtasari
  • Wakili Kipkorir aeleza jinsi alipigana na virusi vya corona baada ya kupatikana nazo
  • Pia alisema kwamba wananchi hawapaswi kulaumu serikali kwa ajili ya matibabu ya virusi hivyo kwa maana bima hailipi gharama ya hospitali
Donald Kipkorir
Image: Hisani

Wakili mmoja wa jijini Nairobi Donald Kipkorir ameeleza jinsi alipigana na maambuizi ya virusi vya corona.

Wakili huyo alisema kwamba alianza kuwa mgonjwa mnamo Novemba 2, 2020.

Kipkorir alisema kwamba hakuwa na dalili za virusi vya corona, huku akisema kwamba mapavu yake tayari yalikuwa yameingiliwa na virusi hivyo wakati alipokuwa nalazwa hospitali.

 

"sikuwa na sina dalili za maambukizi ya corona, nilipatikana navyo,sikuwa na hofu, sikukohoa wala kupiga chafya

Wakati ambao nilipatikana na virusi hivyo mapafu yangu tayari yalikuwa yameingiliwa na virusi,madaktari walianza kunitibu papo kwa hapo ili mapafu yangu yapone viwango vya oksijeni yangu zilikuwa zimepanda na mwili wangu ulipaswa kupigana maradhi hayo

Kwa muda sasa nimekuwa katika hali ya dawa na oksijeni lakini niko sawa natoka hospitalini na kuendelea kupona nikiwa nyumbani."Kipkorir Alisema.

Pia aliwaonya wakenya dhidi ya kutegemea bima ili kulipa gharama ya hospitali kwa ajili ya virusi hivyo.

Donald alisema kwamba kulaumu serikali kwa ajili ya msambao wa corona ni unafiki na uongo kwa maana kuthibiti msambao huo ni jukumu la mtu binafsi.

"Bima hailipi gharama ya hospitali ya virusi vya corona, sijui nilipata aje maambukizi hayo na nina uhakika kwamba sikuambukiza mtu yeyote

Na hakuna serikali mahali popote inaweza lipa, jukumu la la mtu binafsi kuthibiti kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corona

 

Kulaumu serikali kwa ajili ya msambao au matibabu ni uongo na unafiki."

Kufikia jumapili idadi jumla ya walioga dunia ilifikia 1,380 baada ya watu 14 kuaga dunia.