Wandani wa Ruto wamshambulia Kinoti baada ya kufungua kesi za ghasia za 2007/2008

Muhtasari
  • Wandani wake Ruto walisema kwamba kuanzisha kwa kesi hiyo ni njia moja wapo ya kuzuia mazimia yake DP Ruto ya kisiasa 2022
  • Jumatatu Kinoti alikutana na waathiriwa wa ghasia za uchaguzi
  • Alisema idara ya DCI itawachukulia hatua wote waliotekeleza ghasia na uhalifu wakati wa uchaguzi wa 2007/2008

Jumla ya kesi 72 za mauaji ,44 za kuhamishwa kutoka ardhi na vitisho 118 zinazohusiana na ghasia za baada ya uchaguzi tangu machafuko ya mwaka wa 2007/2008 alisema mkuu wa DCI George Kinoti

Akizungumza Jumatatu Kinoti aliahidi kwamba idara yake itafuatilia yote ambayo waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi walimueleza baada ya kukutana nao siku ya jumatatu katika makao makuu ya DCI .

Baada ya habari zake KInoti wandani wake naibu rais kwenye mitandao ya kijamii walimshambuia Kinoti huku wakisema kwamba hii ni njia moja wapo ya kuzuia azimio ya Ruto ya kuwania kiti cha urais.

 

Kinoti alisema kwamba kufunguliwa kwa kesi hizo ni kutokana na malalamishi ya waathiriwa hao ambao walisema kwamba  wanapokea vitisho kutoka kwa baadhi ya wanasiasa.

Kulingana na seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen alisema kwamba kufunguliwa tena kwa kesi hiyo ni kugawanya juhudi za 'system' ili kumleta naibu rais chini.

"Wanataka kuchochea vurugu dhidi ya jamii haswa katika mkoa wa Rift Valley, ili kudhoofisha nguvu zake naibu rais za kisiasa

Wanaeza choma manyumba na kuua watu." Murkomen Aliandika.

Kwa upande wake seneta wa Nakuru Susan Kihika alikuwa na haya ya kusema;

"Natamai hawataua watu, kuchoma manyumba ili kuhalalisha  matamshi yake Kinoti, Ningepinga majaribu ya kushiriki vurugu na kuendelea kuishi kwa amani."

Je maoni yako kuhusu kufunguliwa kwa kesi hizi ni yapi kama mkenya?