Kesi ya mauaji:Polisi aliyeshtakiwa kwa mauaji ya wakili Onesmus Masaku kuzuiliwa hadi Desemba 15

Muhtasari
  • Polisi aliyeshtakiwa kwa mauaji ya wakili Masaku kusalia korokoroni
  • Inadaiwa kuwa polisi huyo alimkata vidole wakili Masaku alipokuwa anataka kumbaka
  • Masaku aliaga dunia Oktoba 8,2020 baada ya kupata majeraha
Onesmus Masaku

Aliyekuwa polisi wa mwanamke ambaye alishtakiwa kwa ajili ya mauaji ya wakili Onesmus Masaku atasalia korokoroni hadi tarehe 15 Desemba ambapo mahakama ya juu ya kaunti ya Machakos itatoa uamuzi wake kuhusu kuachiliwa kwake kwa dhamana.

Nancy Njeri ambaye amekuwa mikononi mwa polisi tangu Oktoba,8,2020 alikuwa mbele ya hakimu David Kenei jumanne ambapo alikataa mashtaka yake na kusema hakumuua mwendazake wakili Masaku kulingana na Citizen Digital.

Timu ya mawakili akiwemo rais wa LSK Nelson Havi anashiriki katika kesi dhidi ya polisi huyo wa zamani.

Wakili Onesmus aliaga dunia Oktoba,18 baada ya kuugua majeraha ambayo alipokea baada ya kushambuliwa na mshukiwa huyo mnamo Oktoba,7 mwaka huu.

Nancy Njeri
Nancy Njeri
Image: courtesy

Masaku aliaga dunia akiwa katika hospitali kuu ya Kenyatta katika kaunti ya Nairobi alipokuwa anapokea matibabu baada ya vidole vyeke kukatwa na Njeri wakiwa nyumbani kwake.

Inadaiwa kuwa wakili huyo alikuwa anataka kumbaka polisi huyo huku akichukua panga na kumkata vidole ili aweze kujikinga naye asitekeleze kitendo hicho.