'Msiache kuomba,' Gavana Sonko awaambia wakenya

Muhtasari
  • Gavana Mike Sonko awashauri wakenya wasiwache kuomba kwa maana Mungu anweza kutenda miujiza
  • Sonko amekuwa na changamoto nyingi tangu mwaka wa 2017 baada ya kuwa gavana wa kaunti ya Nairobi
sonko-mohter-2-e1494853502315
sonko-mohter-2-e1494853502315

Gavana Mike Sonko ana fahamika kwa utajiri wake, gavana huyo kwa muda sasa amekuwa akipitia majaribio mengi huku akinyang'anywa mamlaka ya kusimamia jiji la Nairobi baada ya kupatwa na kesi za kashfa.

Changamoto ya lwanza aliopokea tangu kukalia kiti chake cha ugavana ni baada ya naibu wake Polycarp Igatje kujiuzulu mwaka wa 2018, Januari,12.

Awali kumekuwa na ugomvi kati ya gavana huyo na bosi wa NMS Badi Mohamed.

 

Kwa muda sasa kupitia kwenye mitandao ya kijamii Sonko amekuwa akiwashauri wakenya na neno la Mungu hii leo kupitia kwenye ukurasa wake aliwaambia wakenya wasikome kuomba na wazidi kuomba na kutarajia miujiza kutoka kwake mwenyezi Mungu.

Huu hapa ujumbe wake;

"Usiache kumwomba Mungu mpaka hali yako ibadilike, hata hali yako ikibadilika endelea kumuomba Mungu 

Tunamwomba Mungu atupe faraja nguvu na amani Kwa njia hii Mungu anaweza kukusaidia kuzingatia na kukaa mzuri kushughulikia shida na mapambano yako. Mungu anaweza kukutendea miujiza." Aliandika Sonko.