'Naomba wakenya waunge mkono BBI,'Wetang'ula abadilisha msimamo wake kuhusu BBI

Muhtasari
  • Moses Wetangula awaomba wakenya kuunga mkono BBI
  • Mwanasiasa huyo alikuwa amepinga ripoti ya BBI awali huku sasa akionekana kubadili msimamo wake
Moses Wetangula

Siku chache baada ya rais Uhuru Kenyatta na mwenzake kinara wa chama cha ODM Raila Odinga kuzindua rasmi ripoti ya BBI, jumatano vigogo hao walizindua ukusanyaji wa saini wa ripoti hiyo.

Mmoja wa wandani wa karibu wa Raila Seneta wa kaunti ya Bungoma Moses Wetang'ula alipinga ripoti ya BBI baada ya uzinduzi wake huku akitangaza msimamo wake.

Alikuwa anapinga haya kwa ajili ya ubadilishaji katiba ya mwaka wa 2010.

Hata hivyo siku chache baadaye seneta huyo ameonekana kubadilisha msimamo wake na kuwaomba wakenya kuunga mkono ripoti ya BBI.

Usemi wake unajiri saa chache baada ya uzinduzi wa ukusanyaji saini kufanyika katika ukumbi wa KICC jumatano.

KUpitia kwenye ukurasa wake wa twitter Wetang'ula alikuwa na haya ya kunakili;

"Rasimu ya Muswada wa BBI ni uboreshaji mkubwa kutoka kwa ule uliozinduliwa katika ukumbi wa Bomas

Maswala mengi ambayo mimi, Kalonzo MUsyoka na Farah iliyowasilishwa kutoka kwa mkutano wa viongozi wa vyama vya pol na rais Uhuru Kenyatta yamezingatiwa 

Naomba wakenya wote waunge mkono BBI." Aliandika Moses.