PICHA: Nduguye mcheshi Njugush afunga pingu za maisha

Njugush na nduguye Ngugi
Njugush na nduguye Ngugi
Image: Picha: Kwa hisani

Sio wengi wanaomjua  Ngugi Ndegwa, ambaye ni nduguye msanii na mcheshi, Njugush.

Hii ni kwa sababu ameweza kuyaweka maisha yake mbali na vyombo vya habari huku akiendeleza kazi yake ya uandishi na usanii.

Hapo jana, Ngugi Ndegwa alifunga pingu za maisha na mpenziwe Lily.

Akitangaza habari hizi njema, Njugush alichapisha picha akiwa na bwana Ngugi huku akimpongeza kwa safari hii aliyoianza rasmi hapo jana.

Aliandika;

"Ndugu yangu mpendwa, kwako najivunia sana @ngugi_ndegwa_lepoete leo ilikuwa siku ya kufana sana !!! Hongera wewe na mtu wako !!!!"

Kupitia mtandao wake wa kijamii, Ngugi alichapisha picha yake na mke wake na kumshukuru mungu kwa siku ya kufana.

"Mungu ni mwema!" Aliandika Ngugi.

Soma baadhi ya jumbe za pongezi kwa Ngugi na mkewe;

Kate Actress: CONGRATULATIONS @ngugi_ndegwa_lepoete may God bless your union πŸ™

Judy Nyawira: Congratulations Ngugi & Lily!

Celestine Ndida: Well doneπŸ‘πŸ‘πŸ‘

Marto: congrats bro. Venye tuliongea, next year ni mimi, sitaachwa nyuma.. I'm so happy for you and I wish you a happy and blessed marriage... Well done πŸ‘πŸ‘πŸ‘

Dantei: Congrats bro πŸ‘ŒπŸ‘ŒπŸ‘ŒπŸ’―πŸ’―πŸ’―sisi tuko nyuma bado tunakm β˜ΊοΈβ˜ΊοΈπŸ‘Œ

Tunampongeza Ngugi na Lily kwa kufunga pingu za maisha na kuwatakia maisha mema yenye heri na fanaka.