Bobi Wine aonekana kupiga magoti mbele ya wananchi akifanya kampeni huku siku za uchaguzi zikiwadia

Muhtasari
  • Bobi Wine aonekana kupiga magoti mbele ya wananchi akifanya kampeni

Aliyekuwa msanii wa Uganda na sasa ni mwanasiasa Bobi Wine kupitia kwenye ukursa wake wa twitter alipakia pcha huku akiwa amepiga magoti mbele ya wananchi wa Uganda huku akifanya kampeni.

Zumesalia siku chache ili uchaguzi wa nchi hiyo kuwadia na wananchi kuamua nani haswa atakuwa rais wao.

Bobi Wine awali akiwa kwenye mahojiano alidai kuwa aliponea vifo mara kadha huku akisema kwamba amekuwa akinyunyuziwa risasi endapo yuko katika kampeni.

 

Pia mwanasiasa huyo amekuwa akitiwa mbaroni na kuachiliwa mara kwa mara.

Picha aliopakia kwenye mitandao iliibua hisia tofauti kati ya wanamitandao, Bobi aliandika kuwa ananyenyekea sana kuona wananchi wakipiga foleni katika kampeni yake.

"Ni jambo la kupendeza sana kuona mamia ya watu masikini wanajipanga kuchangia kidogo kama shillingi 1000 (USD 0.27) kwa kampeni

Kujidhalilisha kweli kuona Waganda wengi wanamiliki mapambano haya, kila mmoja akicheza jukumu lake!" Aliandika Bobi Wine.