'Tutakulipa kuwa rais,'Mbunge Richard Onyonka amwambia Raila wakati wa mazishi ya Nyagarama

Muhtasari
  • Mbunge wa Kitutu Chache asema abagusii wamo tayari na wana sababu ya kuunga BBI mkono
  • Alizungumza hayo wakati wa hafla ya mazishi ya gavana wa Nyamira Nyagarama, huku akiwakosoa wanaopinga mchakato huo

Mbunge wa Kitutu Chache, Richard Onyonka akiwahutubia wananchi wakati wa kumpa heshima za mwisho gavana wa Nyamira Nyagarama alisema kwamba wakati umewadia kwa wakenya kumlipa Raila Odinga kwa kazi nzuri ambayo amekuwa akifanya.

Onyonka alisema kwamba kinara huyo amepigania haki ya wakenya na anahitaji kuchukua kiti cha urais wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.

"Mungu akubariki mzee Raila, umeteseka kwa ajili ya hii nchi.umepigania nchi hii na tutakulipa kwa kukuchagua kuwa rais wa jamhuri ya kenya." Alizungumza mbunge huyo.

 
 

Vigogo waliozungumza katika hafla hiyo walisem kwamba wataunga mkono ripoti ya BBI ambayo imekuwa ikipokea ukosoaji mkubwa kutoka kwa baadhi ya wanasiasa.

Pia mbunge huyo akizungumza siu ya Alhamisi,Desemba,24 alisema kwamba kabila ya Aagusii itamuunga na kumshika mkono kinara wa ODM Raila Odinga.

"Hatuangalii nafasi, tunaangalia jinsi pesa zitagawanywa katika kaunti,sisi Abagusii tuna sababu ya kuunga mkono BBI

Tukiangalia katika historia ya taifa makabila chache tu wamekuwa mamlakani tunataka kubadilisha hayo." Aliongeza Onyonko.